YouVersion Logo
Search Icon

Ayu UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki ni kimojawapo cha vitabu viitwavyo “Maandiko ya Hekima”. Kimeandikwa kimashairi. Jina lake latokana na mtu ambaye habari zake zinasimuliwa kitabuni aitwaye Ayubu.
Ayubu alikuwa mcha Mungu, mwenye heri, mali nyingi na hekima. Aliishi Usi iliyoko mashariki ya Palestina. Mwovu alidai kuwa mtu kumwamini, humcha na kumtegemea Mungu kwa sababu anaishi maisha ya heri. Kinyume chake angeliasi (1:9-11; 2:4-5). Mungu aliruhusu masaibu kwa Ayubu ili kupinga madai ya mwovu na kuthibitisha uthabiti wa imani ya Ayubu na kumtegemea Mungu (1:8; 2:3). Katika hali hiyo rafiki zake walimwendea wakidai kuwa maafa yake yalisababishwa na dhambi zake za sirini. Ayubu alifahamu kuwa hakuwa mkamilifu, lakini alikataa hoja za rafiki zake.
Majadiliano kati ya Ayubu na rafiki zake ndiyo sehemu kubwa ya kitabu hiki. Kiini cha mazungumzo ni suala la kumcha Mungu, kuishi kwa uadilifu, maana ya maisha, mateso ya mwanadamu hapa duniani na Mungu anavyoangalia watu wake.
Ayubu akiwa katika shida na machungu makali aliendelea katika imani na kumtegemea Mungu ijapokuwa mara kadhaa alimlalamikia Mungu. Mungu alitoa tamko lake kuhusu malalamiko hayo. Ayubu alikiri kuwa amesema bila kufikiri sawasawa maana Mungu ndiye mweza wa yote. Mwishoni Mungu akambariki Ayubu, akampa zaidi ya aliyokuwa nayo hapo awali na kukemea rafiki zake Ayubu.
Yaliyomo:
1. Utangulizi: Shetani amjaribu Ayubu, Sura 1–2
2. Ayubu ailaani siku ya kuzaliwa kwake, Sura 3
3. Sehemu tatu za mahojiano, Sura 4–27
4. Wimbo wa sifa za hekima, Sura 28
5. Hatima ya mahojiano, Sura 29–31
6. Hoja za Elihu, Sura 32–37
7. Hoja za Mungu, Sura 38–41
8. Maneno ya kufunga, Sura 42

Currently Selected:

Ayu UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy