YouVersion Logo
Search Icon

Isa 3

3
1 # Law 26:26; Yer 37:21; Eze 14:13 Kwa maana, tazama, Bwana, BWANA wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji; 2mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; 3jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na mganga ajuaye uganga sana. 4#Mhu 10:16Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala. 5#Mik 3:1; Kum 28:50; Omb 4:16Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima. 6Mtu atakapomshika ndugu yake ndani ya nyumba ya baba yake, akisema, Wewe una nguo, ututawale wewe; na mahali hapa palipobomoka pawe chini ya mkono wako; 7basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa. 8Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wayachukize macho ya utukufu wake. 9Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu. 10Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao 11Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake. 12Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako. 13BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu. 14#Mt 21:33BWANA ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu. 15Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuseta nyuso za maskini? Asema Bwana, BWANA wa majeshi.
16BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao; 17Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao. 18Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao; 19na pete za masikio, na vikuku, na taji zao; 20na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu; 21na pete, na azama, 22na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko; 23na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji. 24Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri. 25Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani. 26#Yer 14:2; Omb 1:4Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.

Currently Selected:

Isa 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy