YouVersion Logo
Search Icon

Isa 12

12
Shukrani na Sifa
1 # Isa 2:11; Zek 14:20,21 Na katika siku hiyo utasema,
Ee BWANA, nitakushukuru wewe;
Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,
Hasira yako imegeukia mbali,
Nawe unanifariji moyo.
2 # Kut 15:2; Zab 118:14 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
3 # Yer 2:13; Yn 4:10,14 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. 4Na katika siku hiyo mtasema,
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
5Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
6 # Isa 54:1; Sef 3:14; Lk 19:37-40 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.

Currently Selected:

Isa 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy