YouVersion Logo
Search Icon

Gal 3

3
Sheria au Imani
1Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? 2Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 3Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? 4Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. 5Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 6#Mwa 15:6; Rum 4:3Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 # Rum 4:16 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. 8#Mwa 12:3; 18:18; Mdo 3:25Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9#Rum 4:16Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. 10#Kum 27:26Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. 11#Hab 2:4; Rum 1:17; Ebr 10:38Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani. 12#Law 18:5; Rum 10:5Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. 13#Kum 21:23; Rum 8:3; 2 Kor 5:21Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Ahadi kwa Abrahamu
15Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno. 16#Mwa 12:7; 13:15; 17:7; 22:18; 24:7Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. 17#Kut 12:40Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi. 18#Rum 4:14; 11:6Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
Wajibu wa Torati
19 # Rum 5:20; Ebr 2:2; Mdo 7:38,53 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe. 20Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. 21#Rum 8:2-4Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria. 22#Rum 3:9-19; 11:32Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
23 # Gal 4:3; 1 Pet 1:5 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. 24Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25#Rum 10:4Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. 26#Yn 1:12; Rum 8:17Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27#Rum 6:3; 13:14Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28#Rum 10:12; 1 Kor 12:13Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29#Rum 4:13; 9:7Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Currently Selected:

Gal 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy