YouVersion Logo
Search Icon

Kut 15

15
Wimbo wa Musa
1 # Ufu 15:3; Amu 5:1; 2 Sam 22:1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema,
Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana;
Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
2 # Zab 118:14; Isa 12:2; 2 Sam 22:47; Zab 99:5 BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;
Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
3 # Ufu 19:11; Zab 83:18 BWANA ni mtu wa vita,
BWANA ndilo jina lake.
4Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,
Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5Vilindi vimewafunikiza,
Walizama vilindini kama jiwe.
6 # Zab 118:15 BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo,
BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.
7 # Zab 59:13; Kum 4:24; Ebr 12:20; Isa 5:24 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea,
Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
8 # Ayu 4:9; Hab 3:10 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,
Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
9 # Isa 53:12; Lk 11:22 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara,
Nafsi yangu itashibishwa na wao;
Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
10Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
11 # 2 Sam 7:22; 1 Fal 8:23; Zab 86:8; Yer 49:19 Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe?
Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu,
Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
12Ulinyosha mkono wako wa kuume,
Nchi ikawameza.
13 # Zab 78:54 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa,
Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
14 # Yos 2:9; Zab 48:6 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka,
Wakaao Ufilisti utungu umewashika.
15 # Hab 3:7 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa,
Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata,
Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.
16 # Kum 2:25; 1 Sam 25:37; Kum 32:9; Isa 43:1; Yer 31:11; Tit 2:14; 1 Pet 2:9; 2 Pet 2:1 Hofu na woga umewaangukia;
Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe;
Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA,
Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.
17 # Zab 44:2 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako,
Mahali pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae,
Pale patakatifu ulipopaweka imara, BWANA, kwa mikono yako.
18BWANA atatawala milele na milele.
19Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Wimbo wa Miriamu
20 # Amu 11:34; 21:21; 1 Nya 15:16; 1 Sam 18:6; Zab 68:25; 81:2; Yer 31:4 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza. 21Miriamu akawaitikia,
Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana;
Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
Maji Machungu Yafanywa kuwa Matamu
22Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. 23#Hes 33:8; Rut 1:20Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. 24Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? 25#Kut 14:10; 17:4; Zab 50:15; 2 Fal 2:21; 4:41; Yos 24:25; Kut 16:4; Kum 8:2,16; Zab 66:10; 81:7Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko; 26#Kum 7:12; 28:27; Kut 23:25; Zab 103:3; 147:3akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
27 # Hes 33:9 Wakafikilia Elimu, palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na mitende sabini; wakapanga hapo, karibu na maji.

Currently Selected:

Kut 15: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy