YouVersion Logo
Search Icon

Kum 25

25
1Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; 2#Lk 12:48; Mit 19:29; Mt 10:17na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu. 3#2 Kor 11:24; Ayu 18:3Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.
4 # 1 Kor 9:9; 1 Tim 5:18; Mit 12:10 Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.
Ndoa ya Kijamaa
5 # Mt 22:24; Mk 12:19; Lk 20:28; Mwa 38:8; Rut 1:12 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 6#Mwa 38:9Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. 7#Rut 4:7-8Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. 8Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, 9#Rut 4:7; Isa 20:2ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. 10#Mit 6:33; 1 Tim 3:7Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.
Maagizo Mbalimbali
11Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake; 12#Kum 19:13umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako.
13 # Law 19:35-36; Mit 11:1; 20:23; Eze 45:10; Amo 8:5; Mik 6:11 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. 14Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. 15#Kut 20:12Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako. 16#Mit 11:1; 20:23; Amo 8:5-7; 1 Kor 8:9-11; 1 The 4:6; Ufu 21:27Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
17 # Kut 17:8-14; 1 Sam 15:2-9 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; 18#Neh 5:9,15; Zab 36:1; Mit 16:6; Rum 3:18jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. 19#1 Sam 15:3Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.

Currently Selected:

Kum 25: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy