YouVersion Logo
Search Icon

Kum 23

23
Waliokatazwa Mkutanoni
1Aliyejeruhika konde, au aliyekatika tupu yake, asiingie mtu huyo katika mkutano wa BWANA.
2Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.
3 # Neh 13:1-2; 4:3-7; Rut 4:5 Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa BWANA; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa BWANA milele; 4#Hes 22:1-6; Mwa 14:18; Kum 2:29; 1 Sam 25:11; 1 Fal 18:4; Isa 63:9; Mt 10:40,42; 25:41-46; Yos 24:9kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize. 5#Hes 23:7—24:9; Mit 26:2Lakini BWANA, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; BWANA, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda BWANA, Mungu wako. 6#Ezr 9:12Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele.
7 # Mwa 25:24-26; Oba 1:12; Kut 22:21; 23:9; Kum 10:19; Law 19:34 Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake. 8Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa BWANA.
Maagizo kuhusu Usafi, Ibada na Utu
9Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika marago, jilinde na kila neno baya. 10#Law 15:16; Hes 5:2,3; 1 Kor 5:11,13Akiwa kwenu mtu awaye yote asiyekuwa ni tohara kwa ajili ya yaliyomtukia usiku, na atoke nje ya kituo, wala asiingie ndani ya kituo; 11lakini na iwe ikaribiapo jioni, yeye ataoga maji; na jua likiisha kuchwa ataingia ndani ya kituo. 12Tena uwe na mahali nje ya kituo, kwa kutokea nje; 13nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho; 14#Mwa 15:1; Law 26:12; Yer 32:40; 2 Kor 6:16; Kut 3:5kwa kuwa BWANA. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.
15 # 1 Sam 30:15 Usimrudishe kwa bwana wake mtumwa aliyejiponya kutoka kwa bwana wake kuja kwako; 16#Kut 22:21; 23:9; Mit 22:22; Yer 7:6; Zek 7:10; Mal 3:5; Yak 2:6na akae nawe, katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, mahali atakapochagua palipo pema machoni pake; usimwonee.
17 # Law 19:29; Mit 2:16; Mwa 19:5; 2 Fal 23:7 Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume. 18Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.
19 # Kut 22:25; Law 25:36-37; Kum 15:7-11; Neh 5:2,7; Zab 15:5; Lk 6:34 Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba; 20#Law 19:34; Kum 15:10mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
21 # Hes 30:1-16; Mt 5:33; Ayu 22:27; Zab 61:8; Mhu 5:4,5 Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako. 22Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako. 23#Zab 66:13Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.
24 # Mt 12:1; Lk 12:15; 1 Kor 6:10; Kol 3:5 Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako.
25Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako.

Currently Selected:

Kum 23: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy