YouVersion Logo
Search Icon

Kum 14

14
Desturi za Maombolezo Zilizokatazwa
1 # Law 19:28; 21:5; Mwa 6:2,4; Kut 4:22,23; Zab 82:6,7; Yer 3:19; Hos 1:10; Rum 1:10; 8:16; Gal 3:26; 1 Yoh 3:1; Yer 16:6; 41:5; 1 The 4:13 Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa. 2#Kut 19:5-6; Kum 4:20; 7:6; 26:18; Tit 2:14; 1 Pet 2:9; Law 11:45; 19:2; Isa 62:12; Dan 8:24; Rum 12:1Kwa kuwa u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, na BWANA amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.
Chakula Safi na Najisi
3 # Isa 65:4; Eze 4:14; Mdo 10:13; Rum 14:14 Usile kitu cho chote kichukizacho. 4#Law 11:2Wanyama mtakaokula ni hawa ng’ombe, na kondoo, na mbuzi, 5kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; 6na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla. 7Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; 8na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
9Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula; 10na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. 12#Law 11:13Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu; 13na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake; 14na kila kunguru kwa aina zake; 15na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 16na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa; 17na mwari, na nderi, na mnandi; 18na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo. 19Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale. 20Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
21 # Kut 23:19; 34:26; 22:31; Law 17:15; 22:8; Eze 4:14; 44:31; Kut 23:19; 34:26 Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
Maagizo Kuhusu Fungu la Kumi
22 # Law 27:30-33; Hes 18:21; Kum 12:6,17; Neh 10:37 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23#Zab 2:11; 5:7; Mit 3:13; Isa 8:13; Yer 32:38-41; Ebr 12:28Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. 24#Kum 12:21Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; 25ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; 26na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27#Rum 13:4; 15:27; 1 Kor 9:1-14; Hes 18:20; Kum 18:1,2na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
28 # Amo 4:4 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; 29#Kum 10:18; Zab 94:6; Isa 1:17; Eze 22:7,29; Lk 14:12; Ebr 13:2; Kum 15:10; Zab 41:1; Mit 11:24; 19:17; Isa 58:7-12; Mal 3:10; Lk 11:41; 2 Kor 9:6-11na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.

Currently Selected:

Kum 14: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy