YouVersion Logo
Search Icon

Kum 11

11
Thawabu za Utiifu
1 # Zek 3:7 Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake. 2Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na vijana vyenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka, 3#Kut 7:8—12:13na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri; 4#Kut 14:28na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi zao, na magari yao; na alivyowafunikiza maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandamia, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo; 5na mambo aliyowafanyia ninyi barani, hata mkaja mahali hapa; 6#Hes 16:1,31-32; Zab 106:17na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote; 7lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote. 8#Yos 1:6,7Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi mwivukiayo kuimiliki; 9#Kum 4:40; 5:16; Mit 3:1,26; 10:27; Kut 3:8nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali 10#Zek 14:18Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinywesheleza kwa mguu wako, kama shamba la mboga; 11#Kum 8:7lakini nchi mwivukiayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyweshwa maji ya mvua ya mbinguni; 12#1 Fal 9:3nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.
13 # Law 26:3-5; Kum 7:12-16; 28:1-14; 6:17; 2 The 3:5 Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, 14#Law 26:4; Kum 28:12; Yoe 2:23; Yak 5:7ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. 15#Zab 104:14; Yoe 2:19Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba. 16#Ayu 31:27Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; 17#Kum 6:15; 1 Fal 8:35; 2 Nya 6:26; 7:13hasira za BWANA zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo BWANA. 18#Kum 6:6-9Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. 19#Mit 22:6Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 20#Hab 2:2Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; 21#Mit 3:2; 4:10; Zab 72:5; 89:29ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi. 22#Kum 6:17Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye; 23#Kum 4:38; 9:1ndipo BWANA atakapowafukuza mataifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuwapita ninyi. 24#Yos 1:3-5; 14:9; Mwa 15:18; Kut 23:31; Hes 34:3Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu. 25#Kum 7:24; Kut 23:27Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
26 # Kum 30:1 Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; 27#Kum 28:2baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo; 28#Kum 28:15na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
29 # Kum 27:11-14; Yos 8:33-35 Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali. 30Je! Haiwi ng’ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waketio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More? 31Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo. 32Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.

Currently Selected:

Kum 11: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy