YouVersion Logo
Search Icon

Mdo 13

13
Barnaba na Sauli Wateuliwa
1 # Mdo 11:27 Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. 2#Mdo 9:15Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3#Mdo 6:6; 14:23; 1 Tim 4:14; 5:22Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
Mitume Wahubiri katika Kipro
4 # Mdo 15:39 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro. 5#Mdo 12:12,25; 13:13Na walipokuwa katika Salami wakalihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi, nao walikuwa naye Yohana kuwa mtumishi wao.
6Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; 7mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8#2 Tim 3:8Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10#Hos 14:9akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11#Mdo 9:8; Yn 9:39Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. 12Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Paulo na Barnaba wakiwa Antiokia ya Pisidia
13 # Mdo 12:12,25; 15:38 Kisha Paulo na wenziwe wakang’oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu. 14Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. 15#Mdo 15:21Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
16Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, Enyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. 17#Kut 1:7; 12:51; Isa 1:2; Kut 6:1,6; 12:37,41; 14:8Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. 18#Hes 14:34; Kum 1:31; Kut 16:35Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa. 19#Kum 7:1; Yos 14:1Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini; 20#Amu 2:16; 1 Sam 3:20baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli. 21#1 Sam 8:5; 10:21,24Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. 22#1 Sam 13:14; 16:12,13; Zab 89:20; Isa 44:28; Ebr 1:5; 5:5Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. 23#2 Sam 7:12; Isa 11:1Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; 24#Mk 1:4; Lk 3:3Yohana alipokuwa amekwisha kuwahubiri watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. 25#Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:20,27Naye Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.
26 # Zab 107:20; Mdo 13:46 Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa. 27#Mdo 3:17; Yn 16:3Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu. 28#Mt 27:22-23; Mk 15:13-14; Lk 23:21-23; Yn 19:15Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe. 29#Mt 27:57-61; Mk 15:42-47; Lk 23:50-56; Yn 19:38-42Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini. 30#Mdo 3:15Lakini Mungu akamfufua katika wafu; 31#Mdo 1:3akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hata Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu. 32#Mdo 13:23Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa, 33#Zab 2:7ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili,
Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.
34 # Isa 55:3 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,
Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35 # Zab 16:10; Mdo 2:27 Kwa hiyo anena na pengine,
Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.
36 # 1 Fal 2:10; Amu 2:10; Mdo 2:29 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. 37Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.
38 # Mdo 10:43; Hes 15:30; Ebr 9:9; 13:20 Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi; 39#Rum 10:4na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa. 40#Hab 1:5Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii.
41 # Hab 1:5 Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.
42Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili. 43#Mdo 11:23Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu. 44Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. 45#Mdo 13:50; 14:2Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. 46#Mdo 3:26; 18:6; Mt 10:6; Lk 7:30Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47#Isa 42:6; 49:6Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,
Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa,
Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
48 # Mdo 11:18; Rum 8:29 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
49Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. 50Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. 51#Mt 10:14; Mk 6:11; Lk 9:5; 10:11; Mdo 18:6Nao wakawakung’utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. 52Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.

Currently Selected:

Mdo 13: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy