YouVersion Logo
Search Icon

1 Kor 1

1
Salamu
1Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 2#Mdo 18:1; 1 Kor 6:11; Mdo 9:14kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. 3#Rum 1:7Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
4Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; 5kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; 6kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu; 7#Lk 17:30; 2 The 1:7; Tit 2:13hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 8#Flp 1:6; 1 The 3:13; 5:23ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9#1 The 5:24; 1 Yoh 1:3Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
Migawanyiko katika Kanisa
10 # Flp 2:2; 3:16 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 11Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. 12#Mdo 18:24,27; 1 Kor 3:4; Yn 1:42Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. 13Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14#Mdo 18:8; 19:29; Rum 16:23Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; 15mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16#1 Kor 16:15Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine. 17#Yn 4:2; Mt 28:19Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Kristo aliye Nguvu na Hekima ya Mungu
18 # 2 Kor 4:3; Rum 1:16 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19#Isa 29:14Kwa kuwa imeandikwa,
Nitaiharibu hekima yao wenye hekima,
Na akili zao wenye akili nitazikataa.
20 # Ayu 12:17; Isa 19:12; 33:18; 44:25 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 21#Mt 11:25; Lk 8:12Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22#Mt 12:38; Yn 4:48; Mdo 17:18,32Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; 23#1 Kor 2:14; Rum 9:32bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 24#Kol 2:3bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 25#2 Kor 13:4Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
26 # Mt 11:25; Yn 7:48; Yak 2:1-5 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29#Rum 3:27; Efe 2:9mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30#Yer 23:5,6; 2 Kor 5:21; Yn 17:19Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 31#Yer 9:23,24kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

Currently Selected:

1 Kor 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy