YouVersion Logo
Search Icon

1 Kor 2

2
Kumtangaza Kristo Aliyesulubiwa
1 # 1 Kor 1:17 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. 2#Gal 6:14Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. 3#Mdo 18:9; 2 Kor 10:1Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. 4Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, 5#Efe 1:17; 1 The 1:5ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
Hekima ya Kweli ya Mungu
6 # Flp 3:15 Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; 7#Rum 16:25bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 8#Lk 23:34; Yak 2:1; Kol 1:26ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; 9#Isa 64:4lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
10 # Mt 13:11; Mit 20:27 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12#Yn 16:13,14Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 13#1 Kor 1:4Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 14#Yn 8:47; 14:17Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 15#1 Yoh 2:20Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 16#Isa 40:13; Rum 11:34Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Currently Selected:

1 Kor 2: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy