YouVersion Logo
Search Icon

Zekaria Utangulizi

Utangulizi
Maana ya jina Zekaria ni “Bwana amekumbuka”. Zekaria alikuwa kijana wakati alipoanza huduma yake. Zekaria aliwaonya watu waliokuwa wameanza kujenga upya Hekalu kwamba iliwapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia kwa manabii. Aliwahimiza kudumisha uhusiano na Mungu ili wasiiharakishe hukumu ya Mungu. Maono ya nabii Zekaria yalikuwa ya kuwatia moyo wajenzi katika wakati mgumu, na kuwahakikishia kwamba Mungu alikuwa na mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.
Sehemu ya mwisho ya huduma yake, Zekaria alikazia mpango wa maendeleo wa muda mrefu, akionesha kuanzishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa unyenyekevu akileta wokovu, lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani Waisraeli. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisraeli watamtambua Masiya na wataibuka na ushindi, nayo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme.
Mwandishi
Zekaria.
Kusudi
Kuwatia moyo Waisraeli na kuwajulisha mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masiya.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Sura 1–8: mnamo 520–518 K.K.; sura 9–14: mnamo 480–470 K.K.
Wahusika Wakuu
Zekaria, Zerubabeli, Yoshua na Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni.
Wazo Kuu
Ahadi za Masiya na kumalizia ujenzi wa Hekalu.
Mambo Muhimu
Zekaria alieleza juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya adui za Israeli, baraka kwa ajili ya Yerusalemu, na umuhimu wa watu wa Mungu kudumu katika utakatifu. Mungu atawahukumu adui wa Israeli, na Mfalme (yaani Masiya) atakuja.
Yaliyomo
Utangulizi (1:1‑6)
Maono nane ya kinabii (1:7–6:8)
Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (6:9‑15)
Jumbe mbalimbali za hukumu na matumaini (7:1–11:3)
Kuja kwa Masiya na kukataliwa kwake (11:4–13:9)
Bwana yuaja kutawala (14:1‑21).

Currently Selected:

Zekaria Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in