YouVersion Logo
Search Icon

Zekaria Utangulizi

Utangulizi
Maana ya jina Zekaria ni “Bwana amekumbuka.” Yaonekana kama alikuwa kijana wakati alipoanza huduma yake. Zekaria aliwaonya watu waliokuwa wameanza kujenga upya Hekalu kwamba iliwapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia kwa manabii. Aliwahimiza kudumisha uhusiano wa muhimu na Mungu ili wasiiharakishe hukumu ya Mungu. Mfululizo wa maono yalikuwa ya kuwatia moyo wajenzi katika wakati mgumu. Mtazamo wa jumla wa mafunzo wa maono haya manane yaliwahakikishia wajenzi kwamba Mungu alikuwa na mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.
Sehemu ya mwisho wa huduma yake, Zekaria alikazia mpango wa maendeleo wa muda mrefu akionyesha kusimamishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisraeli watamtambua Masiya na wataibuka na ushindi, nayo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme.
Mwandishi
Zekaria.
Kusudi
Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masiya.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Sura 1–8 kati ya 520–518 K.K.; sura 9–14 mwaka wa 480 K.K.
Wahusika Wakuu
Zekaria, Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.
Wazo Kuu
Zekaria anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita watu kwa mwito wa utii. Anaonyesha jinsi watu wanaweza kufanya mambo kwa Roho wa Mungu.
Mambo Muhimu
Zekaria alieleza juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya maadui wa Israeli, baraka kwa ajili ya Yerusalemu, na umuhimu wa watu wa Mungu kudumu katika utakatifu. Mungu atawahukumu adui wa Israeli na Mfalme (Masiya) atakuja.
Mgawanyo
Utangulizi (1:1-6)
Maono nane ya kinabii (1:7–6:8)
Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (6:9-15)
Jumbe mbali mbali za hukumu na matumaini (7:1–10:12)
Kuja kwa Masiya na kukataliwa kwake (11:1–13:9)
Ushindi mwishowe wa Masiya (14:1-21).

Currently Selected:

Zekaria Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy