YouVersion Logo
Search Icon

Malaki Utangulizi

Utangulizi
Malaki maana yake ni “Mjumbe Wangu” au “Mjumbe wa Bwana.” Malaki aliishi baada ya ujenzi wa Hekalu la pili kumalizika. Maisha ya uchaji wa Mungu ya Wayahudi yalikuwa mabaya. Walikuwa wamekengeuka, wakawaoa wanawake wa mataifa mengine, wakaacha kutoa zaka na dhabihu ambayo ni sehemu ya Mungu, hata wakawa wamemwacha Mungu, hali ambayo ilifanana sana na ile iliyokuwepo wakati wa Nehemia.
Mwandishi
Malaki.
Kusudi
Kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao kwa kuziacha dhambi zao ili kurejeza uhusiano wao na Mungu na kuwakumbusha upendo wa Mungu.
Mahali
Yerusalemu na Hekaluni.
Tarehe
Kama 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Malaki, makuhani, na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Mungu anawapenda watu wake hata wakati wanapomwacha na kutomtii. Ana baraka nyingi anazowapa wale walio waaminifu kwake. Upendo wake hauna mwisho.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaonyesha kuwa Hekalu lilijengwa tena, na dhabihu na sikukuu zikarudishwa. Ufahamu wa jumla wa Sheria ulirudishwa tena na Ezra, na kurudi kwao nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea zaidi miongoni mwa makuhani.
Mgawanyo
Upendo wa Mungu kwa Israeli (1:1-5)
Israeli wamtukana Mungu (1:6–2:16)
Hukumu ya Mungu na ahadi yake (2:17–4:6).

Currently Selected:

Malaki Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy