YouVersion Logo
Search Icon

Luka Utangulizi

Utangulizi
Luka alikuwa tabibu. Utangulizi wa Injili ya Luka na ule wa Matendo ya Mitume zinaunganisha vitabu hivi pamoja. Vyote viliandikiwa mtu maarufu wa Kiyunani aliyeitwa Theofilo (maana yake ni Mpenzi wa Mungu). Lugha na mtindo wa Injili ya Luka na pia Matendo unaonyesha kuwa alikuwa mtaalamu mwenye uwezo mkubwa wa kuandika kwa ufasaha, aliyekuwa na elimu ya juu, na asili na mtazamo wa Kiyunani.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba Luka alikuwa mtu wa Mataifa aliyeokoka kutoka Antiokia ya Syria. Aliungana na Paulo huko Troa katika safari ya Paulo ya pili ya kitume. Ingawa kuna kazi nyingine nyingi kumhusu Kristo, Luka alitoa mpangilio na mtiririko wa matukio kama mwana-historia ambaye alikuwa na habari za kina, na mwenye uwezo wa kuandika na kutoa habari za kuaminika.
Mwandishi
Luka.
Kusudi
Kudhihirisha habari sahihi za maisha ya Kristo, na kuthibitisha kwamba Kristo ni Mungu na pia Mwanadamu mkamilifu aliyekuja duniani kwa huduma ya ukombozi wa mwanadamu.
Mahali
Rumi au Kaisaria.
Tarehe
Kama mwaka wa 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu na wanafunzi wake, Elizabeti na Zekaria, Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake, Maria, Herode Mkuu, Pilato, na Maria Magdalene.
Wazo Kuu
Luka anaeleza asili ya Umasihi wa Yesu, na kusudi la huduma yake.
Mambo Muhimu
Luka anadhihirisha kazi na mafundisho ya Yesu, hasa kuelewa mpango wa wokovu, maombi ya Yesu, uhusiano wake na watu maskini, na kudhihirisha kuhusu Roho Mtakatifu. Injili ya Luka ndiyo ndefu kuliko zote.
Mgawanyo
Kuzaliwa kwa Yesu na ujana wake (1:1–2:52)
Kubatizwa na kujaribiwa kwa Yesu (3:14–4:13)
Huduma ya Yesu huko Galilaya (4:14–9:50)
Safari ya Yesu kwenda Yerusalemu (9:51–19:27)
Huduma ya Yesu huko Yerusalemu (19:28–20:47)
Unabii kuhusu mambo yajayo (21:1-38)
Kufa na kufufuka kwa Yesu (22:1–24:53).

Currently Selected:

Luka Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy