YouVersion Logo
Search Icon

Yona Utangulizi

Utangulizi
Yona maana yake ni “Hua.” Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtukia kama mjumbe wa Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mungu aende akawaonye watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli ilhali Ninawi ilikuwa kaskazini mashariki. Yona alipotupwa baharini alimezwa na nyangumi ambaye alimrudisha mpaka pwani ya mashariki ya Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mungu. Alivunjika moyo watu wa Ninawi walipotubu na Mungu akaonyesha rehema zake kwa kughairi na kuahirisha siku ya hukumu.
Mwandishi
Yona mwana wa Amitai.
Kusudi
Kuonyesha ukubwa wa neema ya Mungu, na kuwa wokovu ni kwa watu wote.
Mahali
Israeli, Bahari ya Kati (Mediterania) na Ninawi.
Tarehe
Kati ya 785–760 K.K.
Wahusika Wakuu
Yona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.
Wazo Kuu
Watu wanaposikia neno la Mungu, wanapoamini na kutubu, Mungu huonyesha rehema na kufuta hukumu iliyokuwa inawakabili. Mungu hapendi mtu yeyote aangamie, bali wafikie toba.
Mambo Muhimu
Rehema za Mungu na upendo wa Mungu kwa watu wote.
Mgawanyo
Yona anamtoroka Mungu (1:1-17)
Sala ya Yona na kuokolewa (2:1-10).
Yona aenda Ninawi (3:1-10)
Yona amkasirikia Mungu kwa sababu ya rehema zake (4:1-11).

Currently Selected:

Yona Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy