YouVersion Logo
Search Icon

Yoeli Utangulizi

Utangulizi
Yoeli mwana wa Pethueli maana ya jina lake ni “Bwana ni Mungu.” Nyingi ya kumbukumbu zake katika hiki kitabu na huduma yake hekaluni zinaonyesha kwamba alikuwa nabii aliyetumwa kwa Yuda na Yerusalemu. Kutokana na huduma yake, wengi wamemdhania kuwa nabii wa “kikuhani” (linganisha Yer 28:1, 5) aliyenena neno la kweli la Bwana.
Tukio la unabii wa Yoeli lilikuwa pigo kubwa la nzige waliokula kila jani bichi na hata magome ya miti na mizizi. Akiwaonya watu wamgeukie Bwana kwa njia ya toba, Yoeli anatangaza kwamba “siku ya Bwana” inakuja na italeta hukumu kubwa. Kabla hiyo hukumu haijakuja, Mungu atatuma Roho wake ili kuleta baraka. Yoeli anaelezea kwa undani kuhusu kundi la nzige walioshambulia Palestina. Katika tukio hili aliona ishara ya hukumu ya mwisho na akawaonya watu watubu na kumrudia Mungu.
Mwandishi
Yoeli mwana wa Pethueli.
Kusudi
Kuionya Yuda juu ya hukumu ya Mungu iliyokuwa karibu kwa sababu ya dhambi zake, na kuwahimiza watu wamrudie Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Miaka 835–796 K.K.
Wahusika Wakuu
Yoeli na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Toba husababisha Mungu kughairi mabaya aliyoyakusudia, na badala yake kuleta baraka.
Mambo Muhimu
Pigo la nzige, kuwaonya watu watubu, na tumaini kwa watu wa Mungu.
Mgawanyo
Kuvamiwa na nzige (1:1-12)
Wito wa kutubu (1:12-20)
Maonyo na baraka za Mungu (2:1-32)
Hukumu ya Mungu ya mwisho, na sheria (3:1-12).

Currently Selected:

Yoeli Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy