YouVersion Logo
Search Icon

Wagalatia 5:1-15

Wagalatia 5:1-15 NENO

Kristo alitupatia uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na nira ya utumwa. Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatakuwa na thamani kwenu hata kidogo. Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kupitia kwa sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. Kwa maana, kupitia Roho tunangojea kwa shauku tumaini la haki kwa imani. Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kupitia kwa upendo. Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Ushawishi kama huo haukutoka kwa yule anayewaita. “Chachu kidogo huchachua donge zima.” Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani. Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa. Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe! Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” Lakini mkiumana na kutafunana, angalieni msije mkaangamizana.

Free Reading Plans and Devotionals related to Wagalatia 5:1-15