YouVersion Logo
Search Icon

Ezra 2

2
Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
3wazao wa Paroshi 2,172
4wazao wa Shefatia 372
5wazao wa Ara 775
6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812
7wazao wa Elamu 1,254
8wazao wa Zatu 945
9wazao wa Zakai 760
10wazao wa Bani 642
11wazao wa Bebai 623
12wazao wa Azgadi 1,222
13wazao wa Adonikamu 666
14wazao wa Bigwai 2,056
15wazao wa Adini 454
16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
17wazao wa Besai 323
18wazao wa Yora 112
19wazao wa Hashumu 223
20wazao wa Gibari 95
21watu wa Bethlehemu 123
22watu wa Netofa 56
23watu wa Anathothi 128
24watu wa Azmawethi 42
25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
26wazao wa Rama na Geba 621
27watu wa Mikmashi 122
28watu wa Betheli na Ai 223
29wazao wa Nebo 52
30wazao wa Magbishi 156
31wazao wa Elamu ile ingine 1,254
32wazao wa Harimu 320
33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725
34wazao wa Yeriko 345
35wazao wa Senaa 3,630
36 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
37wazao wa Imeri 1,052
38wazao wa Pashuri 1,247
39wazao wa Harimu 1,017
40 Walawi:
wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74
41 Waimbaji:
wazao wa Asafu 128
42 Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai 139
43 Watumishi wa Hekalu:#2:43 Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54wazao wa Nesia na Hatifa.
55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
58Watumishi wa Hekalu wote nawazao wa watumishiwa Solomoni 392
59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60wazao waDelaya, Tobia na Nekoda 652
61 Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.#2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67ngamia 435 na punda 6,720.
68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000#2:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane 5,000#2:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Currently Selected:

Ezra 2: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy