Mwana wangu, ukikubali maneno yangu,
na kushika maagizo yangu,
ukitega sikio lako kwa kusikiliza hekima,
na kuelekeza moyo wako upate ufahamu,
ukiomba upewe akili,
ukisihi upewe ufahamu,
ukitafuta hekima kama feza,
na kuitaka kama hazina iliyofichwa,
utaelewa maana ya kumwogopa Yawe,
utafahamu maana ya kumujua Mungu.