Kisha Yobu akasimama, akapasua nguo yake, akanyoa nywele zake, akajitupa chini na kumwabudu Mungu, akisema:
Nilikuja uchi katika dunia,
nitaondoka uchi katika dunia.
Yawe amenipa,
Yawe ametwaa.
Jina la Yawe litukuzwe.
Katika mambo haya yote Yobu hakutenda zambi wala hakumushitaki Mungu kuwa na kosa.