Maana, siku nilipowaondoa babu zenu katika inchi ya Misri, sikuwaambia kitu wala kuwapa amri yoyote juu ya sadaka za kuteketezwa na sadaka zingine. Lakini niliwapa amri kwamba waitii sauti yangu kusudi nikuwe Mungu wao, nao wakuwe watu wangu. Niliwaamuru vilevile waishi kama nilivyowaagiza, kusudi wapate uheri.