Hata kama miti ya tini isipochanua maua
wala mizabibu kuzaa zabibu,
hata kama mizeituni isipozaa zeituni
na mashamba yasipotoa chakula,
hata kama kondoo wakitoweka katika zizi
na nyama wa kufugwa kukosekana katika mazizi,
mimi nitaendelea kumufurahia Yawe.
Nitamushangilia Mungu anayeniokoa.