Wakati alipokuwa katika taabu, akamwomba Yawe, Mungu wake rehema. Akajinyenyekeza sana mbele ya Mungu wa babu zake. Alimusihi, naye Mungu akapokea maombi yake na kusihi kwake, akamurudisha Yerusalema katika ufalme wake. Halafu Manase akatambua kwamba Yawe ndiye Mungu.