1
Warumi 10:9
Swahili Revised Union Version
SRUV
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Compare
Explore Warumi 10:9
2
Warumi 10:10
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Explore Warumi 10:10
3
Warumi 10:17
Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Explore Warumi 10:17
4
Warumi 10:11-13
Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Mgiriki; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye ukarimu mwingi kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
Explore Warumi 10:11-13
5
Warumi 10:15
Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Explore Warumi 10:15
6
Warumi 10:14
Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Explore Warumi 10:14
7
Warumi 10:4
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Explore Warumi 10:4
Home
Bible
Plans
Videos