Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu, NakuhitajiMfano

Jesus, I Need You

SIKU 2 YA 7

Ombi:





Yesu, nakuhitaji! Wewe ni Bwana Wangu, Mungu wangu, Mfalme wangu. Unastahili ibada yangu yote. Nisaidia, kwa neema yako, kukujua na kukupenda kwa undani na upendo hata vitu vya ulimwengu huu vikose maana.Nataka kukuabudu wewe na wewe peke yako Sitaki kubadilishwa na utamaduni. Niko ndani yako; nataka kuwa mmoja nawe. Ufunge moyo wangu na wako, na uuweke ukweli wako ndani yangu. Sitaku tu kukufahamu na kufahamu neno lako, nataka niwe na nia yakuiacha dhambi na nikufuate na kulifuata neno lako. Niwezeshe kukuabudu katika roho na kweli.Nahitaji nguvu zako, neeme yako na upendo wako ili bila kujali yale maisha yataleta, nitajibu kila hali, kila mtu, na kila jaribu vile ungejibu kwa utukufu wako. Sitaki kujibu tu kwa nje bali kwa undani, kutoka mto wa maji yaliyo hai Nataka kuwa karibu nawe Yesu, ili roho wako atiririke kutoka kwangu kwa yale yote nitendayo na kusema. Niweze kupata furaha yangu youte ndani yako.Nikutukuze kwa youte nisemayo na kutenda. (Zaburi 42:1-2a; Wagalatia 2:20) ⏎ ⏎ Haijalishi nilipo, ninalofanya, nakala ninayoisoma, au wimbo ninaoimba, nataka akili yangu, nguvu zangu , na moyo wangu ukuzingatie na sio juu yangu na hali zangu. Nakutaka wewe na weke peke yakeHaijalishi kama





nitafualu ama nitaanguka,





nitashinda au kupoteza,





nikiwa tajiri ama maskini,





nikijumuishwa ama kusahauliwa,





nitosheke kwa kujua wewe ni wangu na mimi ni wako.





Nia yangu kuu iwe kukupenda na kupendwa nawe, kukupendeza na kukutumikia wewe. Nisaidie kuiona ndambi yangu, kuiomboleza, na kuikana, kwa neema yako. Nisaidie kuwa na njaa na kiu ya utakatifu.





Bwana Yesu, nipe neema yako, huruma zako, na upendo wako kunisaidia kukuona, kukujua, kukupenda na kuwa mmoja nawe. Asante kwa neno lako linaloniambia nikiuliza chochote kwa jina lako na kulingana na mapenzi yako, hayo utatenda Amen (Yohana 14:13-14)

Kuhusu Mpango huu

Jesus, I Need You

Je, unahisi unamuhitaji Yesu kwa undani? Mpango huu wa maombi wa siku mbili umeundwa kuboresha wakati wako pekee na Yeye na kukusaidia kumlilia Yeye. Unatumika pia kama maombi ya kirafiki kwa sehemu nane ya msururu wa "Y...

More

Tungependa kushukuru Huduma za Thistlebend kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea www.thistlebendministries.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha