Yesu, Nakuhitaji

Siku1 ya 2 • Usomaji wa leo

Ibada
Siku hizi sisi sote tumejijaa wenyewe, bila hata kutambua, lakini kile tunachohitaji zaidi ni kujazwa na Kristo. Mara nyingi ni vigumu kutambua jinsi njia zetu ni tofauti na njia zake kwa sababu, bila kujali ni aina gani ya nyumba tuliyolelewa ndani, ya kristo au isio ya kikristo, kwa sababu ya dhambi inayoishi ndani yetu na kwa sababu tumekua kanisani ndani ya utamaduni huu, tumepata tabia, mifumo ya mawazo, na mafikira kutoka vyanzo vingi zaidi bali na Yesu Kristo, bila hata kujua. ⏎ ⏎Hili lilikuwa lengo la Paulo: "Kwa ajili yangu kuishi ni Kristo" (Wafilipi 1:21). Paulo hakuishi kila mara maisha kwa Kristo. Alianza tu kufanya hivyo wakati Yesu alipokabiliana naye barabarani akielekea Damasko na kumshawishi juu ya dhambi yake, na kuptia neema aliweza kumwona Yesu kwa nani alikuwa (Matendo 9: 1-19). Mfanye Yesu ombi yako na umlilie. Muombe Yesu akupe uwezo wa kumtafuta kwanza kama alivyoamuru katika Mathayo 6: 25-33"Yesu, Nakuhitaji. Siwezi kuishi maisha bila wewe.

Yesu, wewe sio tu wazo, orodha ya matendo au mambo nisifanye, mafundisho, au sababu. Nakuhitaji na nakutamani! Nataka kukujua vyema zaidi kuliko ninavyomjua mtu yeyote - familia yangu, marafiki zangu, rafiki yangu wa karibu - hata mimi mwenyewe. Nataka uwe nami hapa nilipo, sasa hivi. Natamani niweze kukaa karibu na wewe, niutumie mda wangu katika uwepo wako, na nikuuliza maswali yanayo furika akili na moyo wangu. Nataka niwe naweza kukukimbilia, nilaze kichwa changu katika mabega yako, niumwae moyo wangu kwako, na unikumbatie mikononi na unizungumzie ukweli - hata ukweli ulio na ugumu kwangu. Nahitaji msaada wako, neema na huruma zako. Siweki kuishi peke yangu."

Imalize siku ya leo kwa kuomba kupitia Mathayo 6:25-33. Kesho, tutatoa ombi lengine ambalo unaweza omba kila siku ikiwa umeongozwa kuendelea kuomba kwa njia hii