Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 7 YA 30

Baada ya maagizo juu ya sadaka katika Law 1-5, Mungu anamwambia Musa kuhusu wajibu na haki za makuhani katika Law 6-7. Leo tunaelezwa jinsi makuhani walivyoagizwa kuiwakilisha sadaka mbele ya madhabahu. Ilitakiwa kufanyika kwa hali ya unadhifu mkuu, maana ni tendo takatifu na kutakiwa kutolewa kitakatifu. Haruni na wana wake wa kiume ndio wenye jukumu hilo la kuleta upatanisho kati ya Mungu na mwanadamu. Yesu, kama kuhani mkuu wa agano jipya, alikamilisha kazi hii kwa kifo cha msalaba.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz