Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 1 YA 30

Baada ya Mungu kuwatoa Waisraeli huko Misri, na wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi, walianza kumwabudu Mungu kwenye hema ya kukutania. Mungu alikutana nao hapo na kuwapa utaratibu wa kutoa sadaka inayojulikana kama sadaka ya kuteketeza. Mtoaji aliweka mikono juu ya mnyama anayechinjwa kama ishara ya kuhitaji upatanisho na Mungu, kisha mnyama alikufa badala yake. Ukisoma maneno yafuatayo kutoka kwa Rum 6:6-11, tafakari jinsi wale wanaomwamini Yesu na kubatizwa walivyounganishwa na Mungu kupitia kifo cha Yesu cha upatanisho:Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz