Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 19 YA 30

Daudi alisema haya baada ya kusikia mabaya aliyofanya Doegi, Mwedomi (ukitaka kusoma habari hiyo, angalia 1 Sam 22:9-18). Doegi alitunga madhara na kupenda mabaya kuliko mema, hivyo alileta chachu mbaya, hata ikasababisha mauaji ya makuhani:Ulimi wako watunga madhara, kama wembe mkali, Ewe mwenye hila! Umependa mabaya kuliko mema, na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila(m.2-4). Daudi anamtangazia Doegi atakavyoadhibiwa kwa huu uovu. Mungu atamharibu milele.Mungu atakuharibu hata milele; atakuondolea mbali; atakunyakua hemani mwako; atakung'oa katika nchi ya walio hai. Nao wenye haki wataona; wataingiwa na hofu na kumcheka(m.5-6). Tujifunze mambo mawili:1. Tuongee vizuri, tusiwalaumu wengine wala kuwakwaza.2. Tunaposingiziwa kwa uongo na tukaingia katika matatizo, tusihofu. Mungu atatusaidia, kwani ni msaada wetu. Kwa hiyo Daudi anaweza kumaliza zaburi kwa kusema:Mimi ni kama mzeituni umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; mbele ya wacha Mungu wako(m.8-9).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz