Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

[Yesu]akabatizwa na Yohana katika Yordani(m.9).Yohana alikuwa amehubiri kuwa Yesu ni mkuu kuliko yeye:Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu(m.7-8). Kama ni hivi, kwa nini Yesu abatizwe na yeye? Kwa hiyoYohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali(Mt 3:14-15). Ubatizo wa Yohana ulikuwaubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi(m.4). Ila Yesu hakuungama dhambi zake binafsi bali dhambizetu, dhambi za ulimwengu wote. Ushahidi wa Yohana baada ya Yesu kubatizwa ni huu:Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu(Yn 1:29)! Hii ni Injili, ni habari njema kweli! Na utayari wake Yesu ulimpendeza sana Mungu. Kwa hiyo tunasoma kwamba Yesualipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwanawe (m.10-11). Yesu anaanza huduma yake hadharani kwa kutoa Wito:Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili (m.15).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz