Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Mfalme Artashasta anatoa amri ya kuwa wote wa Israeli pamoja na makuhani wao wanaotaka kurudi Yerusalemu waruhusiwe kufanya hivyo. Mfalme anamruhusu pia Ezra kwenda na vitu vyote atakavyohitaji katika nyumba mpya ya BWANA. Anampa kuamua mwenyewe akimwambia:Cho chote kitakachohitajiwa zaidi, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wako, kitakachokupasa kukitoa, kitoe katika nyumba ya hazina ya mfalme(m.20). Hapa tunaona Mungu akiulainisha moyo wa Mfalme na kuondoa upinzani kwa ujenzi huo. Ezra anatambua kuwa hili limewezekana tu kwa ajili ya Mungu, na anaimba wimbo wa kumshukuru Mungu:Ahimidiwe Bwana, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu. Naye amenifikilizia rehema zake mbele ya mfalme, na washauri wake, na mbele ya wakuu wote wa mfalme wenye mamlaka(m.27-28). Je, ukifanikiwa katika kazi zako huwa unakumbuka kumsifu na kumshukuru Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz