Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Ujumbe huu ni habari njema kwetu! Tunaona wazi kwamba mbele ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, nguvu za Shetani hazina uwezo wala nafasi.Yesu ni mkubwa, Shetani ni mdogo. Shetani na mapepo yake lazima watii mamlaka ya Yesu! Kwa nini Yesu aliruhusu wenyeji wa pale wapewe hasara ya nguruwe 2000 walioingia baharini,wakafa baharini(m.13)? Hatujui, lakini huenda Yesu aliona kwamba kutokana na tukio hili la pekee habari ya mwujiza wake haitaweza kusahaulika, bali itaenezwa kwa nguvu katika Dekapoli, eneo la kimataifa. Kwa vyovyote Yesuhakumruhusu [yule aliyekuwa na pepo awe pamoja naye], bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu(m.18-20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz