Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

MsihangaikeMfano

Msihangaike

SIKU 2 YA 5

Uhakika wa Kuhangaika

Watu ambao Kristo alikuwa akizungumza nao katika kifungu hiki walikuwa ni watu wa kawaida kama wewe na mimi ambao walikuwa wakikabiliwa na matatizo ya kifedha na changamoto zinginezo.

Basi hao kama sisi pia, leo, tunahangaika na kusumbukia kodi za upangaji au rehani, kuongezeka kwa gharama za maisha, tuna wasiwasi kuhusu karo za watoto za shule, na gharama za huduma za afya. Zaidi ya hayo, ulimwengu wetu leo, tuna wasiwasi juu ya athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa na vita.

Katika Mathayo 6:24-34, Kristo alitoa funzo hili kama sehemu ya mafundisho yaliyofuata yaliyojulikana kama Mahubiri ya Mlimani mwisho mwa kaskazini ya bahari ya Galilaya, karibu na mji wa Kapernaumu, mahali ambapo Kristo aliishi wakati huo.

Kapernaumu ni mahali palipo kaskazini mwa eneo la Israeli, palipoitwa Galilaya. Nyakati hizo, hapo Galilaya, na pia kote Israeli, ingawaje kulikuwa na matajiri wachache, watu wengi walikuwa ni watu kawaida ambao hangaiko lao kuu lillikuwa kujimudu kimaisha kwa sababu ya mapato duni ilhali gharama za maisha zilikuwa juu sana, madeni, na kodi kubwa. Maisha yao, kama vile yetu leo, yalikumbwa na wasiwasi mwingi na mahangaiko juu ya maisha.

Haya yanatueleza ni sababu gani katika msitari wa 25, Kristo, alitambua ukweli wa hali ya wasiwasi maishani mwa watu wa kawaida, na akawaambia: Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; au miili yenu, mvae nini. Tena katika msitari wa 31, Kristo aliwaambia: Msisumbuke, basi, mkisema, ‘Tule nini?’ au ‘Tunywe nini?’ au ‘Tuvae nini?’

Hivyo, kwa muhtasari wa hoja ya kwanza katokana na kifungu hiki ni kwamba Kristo anawaambia watu aliowafunza, nasi pia, kwamba anafahamu ukweli wa hali ya mahangaiko maishani mwetu, na anajua yote kuhusu hali hiyo, na anaijali, hali hiyo ya mahangaiko ambayo ni hali halisi kabisa maishani mwetu leo.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Msihangaike

Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo w...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha