Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

MsihangaikeMfano

Msihangaike

SIKU 1 YA 5

Mahangaiko

Hivi ndivyo Kamusi inavyofafanua neno hili, Mahangaiko au Wasiwasi juu ya maisha: Uzoefu wa hali ya hofu na kutatizika au wasiwasi juu ya maisha kuhusu hali za matatizo zitakazotukabidhi au zinazoweza kutukabidhi.

Ufafanuzi wa hili neno Mahangaiko unaonyesha kuwa wengi wetu tupo katika hali hiyo hiyo leo ya kuhangaika. Mwaka huu mpya uanzapo, wengi wetu tuna mioyo iliyojaa hofu na inayotatizika kuhusu hali ya dunia yetu, gharama ya maisha, vita katika maeneo mbalimbali, na tishio la vita vya nyuklia, mafuriko, ukame, na yote yanayozushwa na mabadiliko ya hali ya hewa, majanga, na magonjwa ya kuambukiza, na pia matatizo na changamoto tofauti za kibinafsi zinazotukumba.

Mathayo 6:24-34 ni kifungu kifupi cha aya kumi na moja. Lakini neno hili mahangaiko linatokea mara sita katika kifungu hiki kifupi mno. Hii ni kwa sababu, katika kifungu hiki, Kristo anatoa wito kwa watu wa Mungu waache kuhangaika au kufadhaika juu ya maisha yao.

Kristo anatufunza na kutuonyesha katika kifungu hiki, kwanza, Hakika ya uwepo wa kuhangaikia maisha yetu. Pili, tunaona Sababu tunahangaikia maisha yetu. Na tatu, na muhimu zaidi, tunaona jinsi Injili ya Yesu Kristo ndiyo Suluhisho la wokovu kutokana na wasiwasi na kuhangaikia maisha yetu. Pamoja, haya mafunzo yanatupa jibu na msimamo wa injili kuhusu Mahangaiko au Wasiwasi.

Katika mpango huu wa mafunzo ya muda wa siku tano, katika Mathayo 6:24-34, tutachunguza jinsi njia hizi tatu zinaweza kutusaidia katika msimu huu wa matatizo na mahangaiko mengi, na kuturuhusu kuokolewa kutokana na kusumbukia maisha yetu kupitia kwa Injili ya Yesu Kristo.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Msihangaike

Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo w...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha