Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Mara malaika wa Bwana akampiga[Herode], kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho(m.23). Mwanadamu anaweza kujiona na kujifanya mkubwa sana machoni pa watu. Hutokea ikiwa kiburi imeutawala moyo wake. Lakini husahau kuwa uhai wake uko mkononi mwa Mungu! Mbele ya Mungu ni vumbi tu.Changoni vidudu vya tumboni. Vilianza mara moja kumla kuanzia ndani, akafa. Je, umempa Mungu utukufu mbele ya watu kwa mema uliyopokea katika maisha yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/