Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Mwandishi anatukumbusha maana halisi ya Krismasi. Ipo katika uhusiano uliopo kati ya Mungu na Yesu. Katika Yesu, Mungu mwenyewe amefanyika mwanadamu na kuishi kwetu. Yesu amezaliwa na mwanamke kutuonesha jinsi Mungu alivyo. Yesu ametambulishwa kwa alama mbili: a) mng’ao wa utukufu wa Mungu, na b) chapa ya nafsi yake (chapa = picha inayotokea ukigonga mhuri). Kwa alama hizi Yesu anamdhihirisha Mungu. Hii ndiyo maana hasa ya Krismasi: Yesu ndiye uwepo wa Mungu kwetu,Mungu pamoja nasi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/