Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 10 YA 31

Katika somo hili twaona upendo mkuu alio nao Yesu kwa wanafunzi wake. Aliwaona jinsi walivyohangaika. Akaja kuwasaidia. Akawapikia chakula. Wakala pamoja. Hivyo akawahakikishia tena kuwa yu hai na hajawaacha. Pia twatambua jambo lingine muhimu: Yesu siye roho tu. Alifufuka kimwili! Ni rohona mwili. Maana alikula chakula. Katika m.13 imeandikwa kuwaYesu akaenda akautwaa mkate, akawapa, na samaki vivyo hivyo. Katika Lk 24:42-43 ni hata wazi zaidi:Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao.Uthibitisho mwingine ni alama za majeraha Yesu alikuwa nazo mwilini. Alimwambia Tomaso,Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!(Yn 20:26-28). Hata Mbinguni anazo hizo alama. Ndivyo anavyoshuhudia Yohana akiandika,Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa(Ufu 5:6)! Hivi atatufufua na sisi tukiwa na mwili wa utukufu. Huu ni ujumbe wa matumani: Wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake(Flp 3:20-21)!

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha