Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kristo, Malkia Wetu Esta HalisiMfano

Kristo, Malkia Wetu Esta Halisi

SIKU 3 YA 3

Siku ya Tatu – Ibada

Kama ilimbidi Esta kujitambulisha na watu wake ili kuwasaidia, Yesu alijivika mwili wa mwanadamu ili kujitambulisha na sisi kwa kikamilifu, akachukua nafasi yetu msalabani ili kuilipa deni ya dhambi zetu. Na vile vile kama walivyosherehekea wayahudi waliposhindiwa vita vyao na Mungu ili wasiangamizwe, nasi pia tunaweza kusherehekea kwa sababu Yesu ametupigania na kutuweka huru ili tuishi kwa nguvu zake za ufufuo.

Sura za kitabu cha Esta zilizosalia zina matukio makubwa dhahiri ya kusisimua, na ya maajabu makuu. Katika sura ya tano, Malkia huyu myahudi anapigania watu wake kwa kwenda mbele za mfalme Ahasuero kwa ujasiri bila kupewa ruhusa. Kimiujiza, Esta anapokelewa na mfalme na kuhudhuria karamu aliyoindaa Esta. Hapo anaitandaza hadharani mipango ya Hamani bin Hamedatha, na kumsihi mfalme awarehemu watu wake. Hamani ananyongwa. Mfalme Ahasuero anampa Esta mali na urithi wa Hamani, na pia kumpa Mordekai cheo na mamlaka ya Hamani. Ni haki ya kishairi ya kupendeza isiyo na kifani.

Sheria inakataza mfalme Ahasuero kugeuza amri ya Hamani ya kuwaangamiza wayahudi, na kwa hivyo bado wangeuwawa. Lakini Ahasuero anaidhinisha amri ya pili iliyotolewa na Mordekai, ambapo wayahudi wanaweza kupambana na adui zao kutumia vifaa vyovyote walivyoko navyo. Kuna mapinduzi ya kimungu, wayahudi wanashinda na kusherehekea kwa shangwe na vigelegele. Watu wa mataifa mbalimbali walibadilisha dini kwa sababu ya matokeo hayo - jinsi wanaomchukia Mungu hugeuka na kumkubali Yesu kwa vile ameingilia kati maishani mwetu kimaajabu.

Tena, haya yote yana uvumi wa injili. Yesu aliishi katika jumba la kifalme la juu kuliko yote, lakini aliamua kwa hiari yake mwenyewe kuiacha nyuma ili kuingilia kati kwa niaba yetu hapa ulimwenguni (Wafilipi 2:5-11). Na zaidi, Yesu hakufanya hivyo kwa kuhatarisha maisha yake tu, kama vile alivyofanya Esta. Yesu aliyatoa maisha yake sadaka. Esta alisema, “nami nikiangamia, niangamie.” Yesu aliposema, “Baba yangu ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe,” alimaanisha, “Nikiangamia, niangamie.” (Mathayo 26:42). Esta alihatarisha maisha yake ili kununua maisha ya watu wake. Yesu aliyatoa maisha yake ili kuyaokoa maisha yetu, na tunaweza kusema kwa ujasiri na kwa uhuru tunaweza kumkaribia Mfalme wetu wakati wowote.

Hadithi ya kitabu cha Esta kwa ukamilifu – uhamishoni, tishio la mauaji ya kimbari, uokovu, kurudi kutoka uhamishoni – kumefanana na simulizi kuu ya biblia kutoka Mwanzo hadi Ufunuo, ambapo kwa viwango vinne tunapata uumbaji, kuanguka, ukombozi, na uumbaji upya. Kama vile wayahudi walikombolewa wasiangamie kupitia kuingilia kati kwa Esta, na hatimaye wakarudi Yerusalemu kutoka uhamishoni, nasi pia tumekombolewa na Yesu Kristo, aliye kwetu Esta wa kweli na bora zaidi. Haijalishi leo kukutana na ugumu wa maisha ya ukristo hapa uhamishoni mwa ulimwengu huu uliopotoka, tunaipeza sherehe itakayokuwa yetu humo Yerusalemu mpya ambapo hapatakuwa na kilio au majonzi, uchungu, magonjwa au mauti. Na iwe kwamba ukweli wa injili hii tukufu iwape imani na ujasiri, haijalishi hali gani mnayopitia.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kristo, Malkia Wetu Esta Halisi

Kitabu cha Esta ni hadithi ya kushangaza ya ujasiri na upendo ambayo inatuelekeza kwenye hadithi ya Yesu. Katika mpango huu wa siku tatu, Dk. Kwasi Amoafo anachunguza jinsi hadithi ya Agano la Kale ya Esta inavyofanana n...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha