Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kristo, Malkia Wetu Esta HalisiMfano

Kristo, Malkia Wetu Esta Halisi

SIKU 2 YA 3

Siku ya Pili – Ibada

Hadithi ya Esta inatukumbusha ya kuwa sote tunazaliwa na kuingia ulimwengu huu tukiwa tumerithi mauti bila uwezo wa kuugeuza urithi huo. Hadithi yake pia inatukumbusha kwamba Yesu alijivisha mwili wa mwanadamu kama sisi ili kujitambulisha nasi kwa hali yetu ya udhaifu wa kiroho.

Tunaanza somo letu mahali ambapo hadithi ya kitabu cha Esta inasimulia jinsi Wayahudi wote nchini Uajemi walikuwa katika hali ya majonzi na huzuni kuu, kufunga na hali ya magunia pamoja na majivu kwani msiba mkuu uliwakumba kufuatia amri ya Hamani alipoamrisha mauaji ya kimbari (Esta 4:1-3). Mordekai naye anafanya vivyo hivyo hapo hapo langoni mwa hekalu ya Mfalme ili aonekane. Esta anafahamishwa juu ya jambo hili, naye akapeleka ujumbe kupitia msaidizi wake kwa Mordekai kumuuliza anachokifanya. Esta anajulishwa hali kuhusu mpango muovu wa Hamani kuwaangamiza watu wake. Hapo Mordekai anatuma ujumbe kwa binamu yake Esta akimsihi asimame kwa niaba ya watu wake Wayahudi dhidi ya uovu wa Hamani kwa kwenda mbele ya Mfalme akiomba awatetee kesi yao. Esta anajibu kwa kifupi, “una kichaa?” Kisa na maana ni kwamba mtu yeyote anayekwenda mbele ya Mfalme bila kuitwa anahukumiwa kifo. Lakini Mordekai anasisitiza na kumkumbusha Esta ya kwamba cheo chake spesheli chenye nguvu katika ikulu, na kumtia moyo kwa maneno haya, “…nani ajuaye kame wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo.”

Mungu amemuweka Esta katika kiti cha enzi wakati ambapo Wayahudi wamekumbwa na janga la kuuangamizwa, na cheo chake kina uwezo wa kuwaokoa. Wakati huo, Esta alikuwa amemaliza miaka minne ya umalkia bila mtu yeyote katika afisi ya ufalme kufichuwa siri eti yeye ni myahudi. Esta amejiweka katika hatari kubwa kujitambulisha na watu wake lakini anaelewa kuwa hiyo ndiyo njia moja pekee ambayo atakavyoweza kuwasaidia. Esta anarudisha ujumbe kwa Mordekai, akimuuliza awakusnye Wayahudi wote eneo la Shushani wakafunge juu yake atakapojitayarisha kumkaribia mfalme Ahasuero.

Tena, tunamuona Yesu katika hadithi hii. Kama Esta, Yesu hakutambulika yeye kweli ni nani (Yohana 1:10-11). Kama Esta, ambaye alijishusha kwa kujitambulisha kabisa na watu wake, Yesu alikuwa mfano kwa kila hali kama sisi kupitia kuzaliwa kwake kama mwanadamu, ili ajitambulishe nasi na kututetea kesi yetu mbele za Mfalme wa Wafalme (Waebrania 2:14-18).

Pengine, katika hali yako ya sasa, unahisi kwamba Mungu haoni unayoyapitia, au hajali. Tafadhali jua ya kwamba chochote unachokipitia au kinachokukabili sasa hivi, Yesu anajitambulisha nawe kwa hali na njia zako zote kikamilifu. Anakuona, anakupenda, na ana uwezo wa kukukomboa.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Kristo, Malkia Wetu Esta Halisi

Kitabu cha Esta ni hadithi ya kushangaza ya ujasiri na upendo ambayo inatuelekeza kwenye hadithi ya Yesu. Katika mpango huu wa siku tatu, Dk. Kwasi Amoafo anachunguza jinsi hadithi ya Agano la Kale ya Esta inavyofanana n...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha