Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Hekima Ya KirohoMfano

Hekima Ya Kiroho

SIKU 2 YA 3

Ni lazima tutafute hekima ya kiroho kama vile hazina iliyofichwa (Methali 2:18; Ayubu 28:12 - 28).

Methali 2 inarekodi himizo la Sulemani kwa mwanawe kutafuta hekima kama fedha na kuitafuta kana kwamba ni hazina iliyofichwa (2:4). Mara nyingi tunakosa upambanuzi katika kufanya maamuzi yetu kwa sababu sisi ni wavivu sana hata hatuchukui muda kutafuta upambanuzi kwa kile ambacho Mungu angetaka tufanye. Kwa Sulemani, lengo la kutafuta na kuchimba kwa ajili ya kupata hekima lilikuwa kwamba Bwana hutoa hekima:

Kwa kuwa Bwana huwapa hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu (Methali 2:6).

Kwa maneno mengine, hekima ya kiroho inapatikana tunapotafuta mtazamo wake Mungu (au ujuzi wa Mungu) kwa kujifunza Neno lake. Kisha Roho Mtakatifu anatumia ujuzi huu wa Maandiko kwa hali maalum na maswali tunayokutana nayo tunaposafiri maishani.

Tunapotafuta hekima ya Mungu kwa kujifunza na kukariri Maandiko, tutaona, kama mtunga Zaburi alivyofanya, kwamba Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu (Zaburi 119:105).

“Hazina yako iliyofichwa” unayochimba ni ipi? Je, unatafuta kwa bidii hazina ya kumjua Mungu kupitia Neno Lake na kupata hekima yake ya kiroho kwa ajili ya maisha yako?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Hekima Ya Kiroho

Safari zetu katika maisha mara nyingi zinaweza kuhisi kama barabara nyembamba, yenye hila. Hekima ya kiroho ni njia ya Mungu ya kushughulikia safari yetu ya maisha iliyopinda pinda, na isiyonyoofu. Mpango huu wa siku tat...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha