Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Hekima Ya KirohoMfano

Hekima Ya Kiroho

SIKU 1 YA 3

Hekima ya kiroho inatokana na kuwa na mizizi katika maarifa yetu ya Mungu (Waefeso 1:17).

Ombi la Paulo kwa ajili ya Wakristo wa Efeso lilikuwa kwamba Mungu awape roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua Yeye. Kisha Paulo alieleza ujuzi huu mkuu zaidi wa Mungu kama kujua tumaini la mwito wake, utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu, na ukuu usio na kipimo wa uweza wake kwetu sisi tunaoamini (Waefeso 1:18 – 20).

Hekima ya kiroho inaweza fafanuliwa kama, kufanya maamuzi yanayotegemea maoni na mtazamo wake Mungu. Tunapoendelea kumjua Mungu kwa undani zaidi, tunapata mtazamo wake kuhusu hali zetu na kupata hekima Yake ya kiroho kwa maamuzi yetu.

Je, unaweza kuelezea vipi barabara ambayo umekuwa ukisafiria hivi majuzi katika safari yako ya maisha? Je, unakabiliwa na maamuzi magumu na misukosuko na hali iliyojipinda pinda? Tulia sasa umuombe Mungu hekima yake kwa hali na maamuzi yanayokukabili.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Hekima Ya Kiroho

Safari zetu katika maisha mara nyingi zinaweza kuhisi kama barabara nyembamba, yenye hila. Hekima ya kiroho ni njia ya Mungu ya kushughulikia safari yetu ya maisha iliyopinda pinda, na isiyonyoofu. Mpango huu wa siku tat...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha