Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 12 YA 31

Ushuhuda wa wazi wa Yohana kwamba Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, na unyenyekevu wake binafsi kwa Yesu, uliamsha hamu ya wanafunzi wake kumtafuta Yesu. Kama tunavyosoma katika m.37, wale wanafunzi wawili wakamsikia [Yohana] akinena, wakamfuata Yesu. Je, unafahamu waliona nini kwa Yesu hawa wawili? Waliona uzuri uliowafanya wasinyamaze, na hawakunyamaza. Andrea akampeleka Petro, ndugu yake, kwa Yesu. Filipo, jirani yao, naye akamleta Nathanaeli kwa Yesu. Twende kwa Yesu, mimi na wewe. Ameahidi kutufungulia malango ya mbinguni, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu (m.51).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha