Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 23 YA 31

Tusiongeze wala tusipunguze lolote kwa Neno la Mungu, maana matokeo ya kufanya hivyo ni mabaya sana (m.18-19, Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki). Yote tunayohitaji kuyajua kwa ajili ya wokovu, tumefunuliwa, nayo yatatimia hakika. Kwa hiyo Bwana Yesu anakaza mara ya tatu: “Naja upesi.” Angalia itikio la Yohana katika m.20 anasema, “Amina; na uje, Bwana Yesu.” Kwa wakati mmoja huonyesha imani, ombi na hamu ya kuwa pamoja daima na Bwana wake mpendwa. Neema ya Bwana Yesu iwe nawe unapofanya maamuzi juu ya maana ya ujumbe wa Kitabu cha Ufunuo katika maisha yako!

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu u...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha