Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Biblia i HaiMfano

La Biblia está viva

SIKU 5 YA 7

Biblia Hugawanya Giza

Diya hakutaka chochote kinachohusiana na Ukristo. Lakini 2017, rafiki mpendwa wa Diya alitoa ushuhuda wake kanisani kwake New Zealand. Diya alijitokeza kumtia moyo... na akaendelea kuja. Aliyatoa maisha yake kwa Yesu baadaye mwaka ule, kabla hajahamia India.

Akitembea katika imani kwenye nchi mpya pasipo jamii ya wakristo alichoka, na Diya hatimaye alishushwa moyo kiasi kwamba alikuwa anasikia uvivu kuamka kila siku.

“Nilikuwa mpweke na nikakuta ni vigumu kushirikiana na watu. Nilikosa upekee na uhuru nilipohamia India, na mawazo mengi mabaya yaliingia akilini mwangu. Lakini mpaka pale nilipoweza kuungana na Maandiko katika YouVersion ndipo nikabadili namna ya kufikiri.” 

YouVersion ilimpatia Diya njia ya kuunganika na Wakristo wengine na kujifunza kwao kupitia mipango ya Biblia. Na toka 2018, alimaliza mipango 428. 

Kila Diya alipokuwa na swali, alifungua app ya YouVersion na kutafuta mipango inayohusiana na somo analolitaka. Na kadri alivyosoma mipango, ndivyo imani ilivyokua. 

“Wakati fulani nitaanza mipango 11 kujaribu na kuzama katika imani. Ni nafasi ya kujifunza kutoka kwa watu waliokutangulia na kutiwa moyo nayo. Nimekuwa najifunza kwamba siko peke yangu katika mahangaiko haya. Naweza kuwasikia watu waliopitia mfadhaiko na kushinda, na ilinisaidia kutambua kwamba wafuasi wa Yesu wanapambana na afya ya akili pia.” 

Sasa, Diya anapojisikia mpweke, amefadhaika, au ametengwa, anaweza kubaki katika ahadi za Mungu na kushinda mawazo yote anayokuwa nayo kinyume na Yesu aliyosema juu yake. 

“Wakati mwingine, unapofadhaika, unahitaji neno tuu. App ilikuwa ni 'njia ya mkato' iliyonisaidia kuitazama imani yangu na Biblia. Teknologia ni chombo kizuri sana kinachoweza kuunganisha na imani yetu. Sidhani kama ningekuwepo kama nisingepata njia ya kuunganishwa na Yesu, kwa sababu nyakati zile kweli zilikuwa ni, za giza sana na Yeye alikuwa ndiyo chanzo pekee cha Nuru niliyokuwa nayo... na bado ninayo.”  

Kwa sababu ya nguvu ya neno la Mungu, kutengwa kunaweza kubadilishwa kuwa kuunganika, na tumaini linaweza kupatikana katikati ya mgawanyiko.

Angalia habari ya Diya kwa muda, na tumia muda kuzungumza na Mungu kuhusu majira uliyopo sasa. Unapofanya hivyo, muombe Mungu akufunulie ukweli kuhusu hali yako, na ndipo utafuta maandiko yake kuhusu tumaini na kutia moyo. Ruhusu mwanga wake kugawanya giza katika maisha yako.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

La Biblia está viva

Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jin...

More

Mpango huu wa mwanzo wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha