Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 1 YA 31

Katika Eze 39:29 Mungu aliahidi kujenga “nyumba ya Israeli”, akimwaga Roho Mtakatifu juu yake: Sitawaficha uso wangu tena; kwa maana nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU. Kuanzia Eze 40 Ezekieli anafunuliwa utekelezaji wa ahadi hiyo na matokeo yake. Kama Mungu alivyosema na Ezekieli, anatuambia na sisi: Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonyesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuonyeshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli (m.4). Mungu anaweza kutuonya na kutukumbusha, na zipo pia nyakati ambapo kupitia viongozi wetu wa kanisa tunaelekezwa tumjengee Mungu kanisa. Tusiifanye migumu mioyo yetu tukiisikia sauti ya Mungu. Badala yake, tumshukuru na kumtii. Naye atatujenga kwa upya.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mun...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha