Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Silaha ya MunguMfano

The Armor of God

SIKU 2 YA 5

Paulo hakuwa anaomba katika maombi yake kwamba waamini wa Efeso wapokee wingi wa urithi wa utajiri wa kiroho, baraka, nguvu, na mamlaka, bali waweze kutambua kwamba ulikuwa ni wao. Kama wakristo, tayari walikuwa navyo vyote hivyo, kama tufanyavyo sisi. Lakini mpaka watakapotambua, itawafaa nini?



Kwa uhakika, silaha za kiroho anazozielezea katika Waefeso 6 ni marudio tuu ya-- njia tofauti ya kuelezea-- kile Paulo amekuwa akielezea katika sehemu ya kwanza ya waraka. Wanawezaje "kuvaa" au "kubeba" vitu ambavyo hawajui kama wanavyo? Hatua ya kwanza kwao--hatua ya kwanza kwetu--katika kutumia rasilimali za kiroho ambazo tumepewa ni kuwa na macho ya kiroho wazi ili tuweze kuziona.



Habari ya Elisha na mtumishi wake aliyekuwa haoni katika 2 Wafalme 6 ni moja ya habari nazozipenda katika Biblia. Kilicho mbele yao ni vita ambayo inataka kuanza kati ya mfalme wa Shamu na taifa la Israeli.



Mtumishi wa Elisha alipata kuona. Mwanzoni, aliweza kuona maadui, ambao walimfanya kutokuwa na jingine zaidi ya hofu na mashaka.



Lakini ghafla akabadilishwa kwenye ukweli wa kiroho: alikuwa na vingi zaidi na vyote vikifanya kazi kwa ajili yake kuliko alivyotarajia. Vile ambavyo macho yake ya nyama yaliweza kuona havikulingana na vile ambavyo walikuwa hawavioni. Maombi ya Elisha yalimfanya ajue rasilimali na nguvu zote za upande wake kwa ajili ya kupigana na adui.



Ili kuwa na ujasiri na kuwa mshindi, unatakiwa kuwa na uwezo wa "kuona".



Katika Waefeso 1, Paulo amasisitiza kidogo juu ya karama za Mungu alizotupa. Kuna zaidi ya hizo, na kila moja inaungana vizuri na silaha zako za kiroho. Ufunguo wa kwanza kuzielewa jinsi zote zinavyofaa katika uwezo wako wa kumshinda adui ni maono. Huwezi kuzitumia kama huwezi kutambua kikamilifu, kama huwezi kujua kama zinapatikana na umuhimu wake katika kupigana vita ya ushindi dhidi ya adui.



Ushindi unaanzia hapa. Unaanza leo. Unaanza kwa maombi ya maono. Kwa hiyo ungana na Paulo katika kumwomba Bwana kufungua macho yako zaidi ili usihisi tuu kazi za adui, lakini uwe unafahamu kwa uhakika juu ya kile Mungu amekupa kumnyang'anya na kumshinda katika maisha yako

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

The Armor of God

Kila siku, vita isiyoonekana inapiganwa kukuzunguka--haionekani, haisikiki, lakini bado unaihisi katika maisha yako yote. Adui wa kishetani aliyejitoa kuleta uharibifu kwa kila kitu muhimu kwako: moyo wako, akili yako, n...

More

Tungependa kuwashukuru Priscilla Shirer na LifeWay Christian Resources kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.lifeway.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha