Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Mungu Huzungumza Kwa Njia Nyingi
Mimi, [ambaye] nisemaye kwa haki… (ISAYA 63:1)
Katika andiko la leo, Mungu anatangaza kuwa anazungumza, na anapozungumza, anazungumza kwa haki. Tunaweza kutegemea anachosema kila mara tukijua kwamba ni cha kweli. Mungu huzungumza nasi kwa njia nyingi ambazo hujumlisha pasi kubanwa: kwa Neno lake, viumbe asili, watu, hali, amani, busara, uingiliaji wa kiungu, ndoto, maono, na kile ambacho wengine wanaita “ushahidi wa ndani,” ambao unaelezwa vizuri kama “kujua” kwa mioyo yetu ya ndani. Anazungumza pia kwa kile ambacho Biblia inaita “sauti ndogo tulivu,” ambayo naamini kwamba pia inarejelea ushahidi wa ndani.
Mungu huzungumza pia kupitia kwa dhamiri, kupitia kwa haja zetu na kwa sauti inayosikika, lakini kila mara kumbuka kwamba anapozungumza, anachosema huwa cha kweli wakati wote na huwa hakipingani na Neno lake lililoandikwa. Ni nadra kusikia sauti inayosikika ya Mungu, ingawa hufanyika. Nimesikia sauti inayosikika ya Mungu mara tatu au nne katika safari yangu ya maisha. Niliisikia mara mbili nikiwa nimelala ikaniamsha kwa kuniita tu kwa jina langu. Nilichosikia tu ni, “Joyce,” lakini nilijua Mungu anazungumza. Hakusema alichokuwa akitaka, lakini nilijua bila kufikiri kwamba alikuwa akiniita kumfanyia kitu maalum, ingawa uwazi haukutokea hapo kwa muda wa miaka mingi.
Ninataka kukuhimiza kumwambia Mungu akusaidie kusikia sauti yake kwa njia yoyote anayochagua kuzungumza nawe. Anakupenda; Ana mipango mizuri juu ya maisha yako; na anataka kuzungumza nawe kuhusu mambo haya.
NENO LA MUNGU KWAKO WEWE LEO
Mungu huzungumza kwa njia nyingi; kumbuka tu- hawezi kwenda kinyume na Biblia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!
More
Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/
Mipangilio yanayo husiana

Ibada juu ya Vita vya Akilini

Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

Upendo Wa Bure

Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021
