Kutafuta Njia ya Kumrudia Mungu

Siku1 ya 5 • Usomaji wa leo

Ibada
"Inatakiwa kuwa na mengi"

Je, huwa una hisi kuwa unatafuta kitu maishani ambacho hakitakukidhi kikamilifu? Usipuzilie mbali hisia hiyo. Ni kutoka kwake Mungu.

Hatuzungumzii kuhusu madawa ya kulevya, ingawaje kunya pombe ni njia hakika za kutafuta vitu bure. Lakini tumewajua "watu wazuri wa kanisani" ambao huketi kanisani kila wiki—au wanaohubiri katika mimbari kwa watu hao—ambao wanajihisi kuwa mbali na Mungu, "Wamefanikiwa" au "wako pamoja" au "wenye haki" kwa nje, lakini wanamkosa Mungu kwa undani. Wanajishughulisha na mambo na kazi za kidini, shule, au familia, lakini Wanatamani Mungu awahisi.

Hiyo hali ya kumtaka Mungu ni muamko wa kiroho wa kwanza kwa sisi wote ambao tunatafuta njia ya kumrudia Mungu. "Kuna zaidi ya hayo."

Unapotamani upendo ambao ni wa kina na unaotosheleza, unapotaka kujipatia kwa kitu ambacho kitaleta mabadiliko ya ukweli, au unapotafuta majibu ya maswali magumu ya maisha, unamtafuta Mungu. Una chaguo mbili: unaweza endelea kutafuta ili kujitosheleza kwa njia zako mwenyewe, au unaweza kumtazamia Yule ambaye alikupatia hizo hisia za kutamani kutoka mwanzo.

Hamu yetu ya upendo wa ukweli inaturudisha hadi jinsi mwanadamu alivyoumbwa hapo mwanzo. Mungu alikusudia kwamba tushuhudie upendo wake moja kwa moja kutoka kwake na kupitia wengine tunaohusiana nao kwa njia nzuri. Kile tunachohamu nacho, sio tu Mungu anacho bali pia Mungu ni hicho kitu. Yeye ni upendo na anatufuata na upendo.

Tumeyasikia yakisemwa kuwa kila anayebisha mlango wa danguro anamtafuta Mungu. Ikiwa unabisha mlango wa tabia na husiano za kibinafsi na za uharibifu, unaweza kuwa umefika hatua muhimu katika safari yako ya kumrudia Mungu. Kwa nini? Kwa sababu masikitiko utakayo kuwa nayo kwa kuchagua vitu nafuu mbadala yatakufanya uanze kuwaza ni wapi utapata upendo wa kweli. Je, utamuacha Mungu ajaze hamu yako ya kupenda na kupendwda?

Ni nini shughuli zako za wiki hii zanaashiria kuhusu unachofikiria kitakutosheleza?